Mtandao wa Tor inategemea watu wanaojitolea kuchangia kipimo data. Kadiri watu wengi wakiendesha rilei mtandao wa Tor utakuwa bora zaidi. Mtandao wa sasa wa Tor ni mdogo sana ikilinganishwa na idadi ya watu wanaohitaji kutumia Tor ambayo nikumaanisha kuwa tunahitaji watu waliojitolea zaidi kama wewe ili kuendesha rilei.
Kwa kuendesha rilei ya Tor unaweza kusaidia kutengeneza mtandao wa Tor:
- haraka (na kwa hivyo inaweza kutumika zaidi)
- imara zaidi dhidi ya mashambulizo
- imara zaidi katika kesi ya kukatika
- salama kwa watumiaji wake (kupeleleza rilei nyingi ni ngumu kuliko chache)
Uendeshaji wa rilei unahitaji ustadi wa kiufundi na kujitolea, ndiyo maana tumeunda rasilimali nyingi ili kusaidia waendeshaji wetu wa rilei.

Aina za rilei kwenye mtandao wa Tor
Bridges, guards, middle relays, and exits all serve important functions in the Tor network. Learn about the different relays you can run.
Mahitaji ya rilei
Mahitaji ya rilei ya Tor hutegemea aina ya relay na kipimo data wanachotoa. Pata maelezo zaidi kuhusu mahitaji mahususi ya rilei.
Nadhari ya kiufundi
Jinsi ya kuchagua mtoaji mzuri wa upangishaji, ni aina gani ya AS na anuwai ya Mfumo wa Uendeshaji.
Usanidi wa kiufundi
Jinsi ya kusanikisha na kusanidi kila aina ya rilei: kiungo, ulinzi, kati na kutoka.
Jumuiya na vyanzo vya kisheria
Jinsi ya kujihusisha na jumuiya ya waendesha relay za Tor, kushauri juu ya majibu ya malalamiko ya unyanyasaji, na jinsi ya kuanzisha shirika litakalojihusisha na uendeshaji wa relay.
Kupata msaada
Jinsi ya kupata usaidizi ukikumbana na maswala
Jihusishe na waendeshaji wa rilei wengine
Rasilimali bora kuliko zote ni jumuiya hai ya waendeshaji wa rilei kwenye orodha ya barua pepe ya rilei za tor na kwenye IRC #rilei za tor katika irc.oftc.net.
Orodha ya barua ya waendeshaji wa rilei